Askari wa Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza, John Nyange ameripotiwa kuuawa kwa kuchomwa kisu katika eneo la baa ya Villa Park jijini humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa askari huyo aliuawa na mtu aliyekuwa na uadui naye ambaye ni fundi ‘computer’ aliyetajwa kwa jina la Magina Hussein. Alisema kuwa marehemu alikuwa anamdai fundi huyo ‘kompyuta mpakato’.

Kwa mujibu wa taarifa yake, Kamanda Msangi amesema kuwa Magina alimchoma shingoni marehemu na kitu chenye ncha kali akishirikiana na wenzake watano. Askari huyo alifariki njiani wakati akikimbizwa hospitalini.

Jeshi hilo tayari limemtia mbaroni Magina Hussein na wenzake watano na wanaendelea kuhojiwa kabla kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.

Kamanda Msangi ameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi kutochukua sheria mikononi kwa kuwapiga watu wengine kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai. Aliwataka kufuata sheria zilizowekwa ili kuepusha vifo vinavyoweza kuepukika.

Hospitali ya Manispaa Mpanda Kuboreshwa
Audio: Lema amjimbu Waziri Nchemba kuhusu ‘kutotikisa kiberiti cha gesi’