Askofu wa Kanisa Katoliki, Mhashamu Evarist Chengula amewataka Wakristo wote nchini kujipanga kumchagua kiongozi anayefaa katika uchaguzi wa mwaka 2019 wa Serikali za mitaa.

Akihubiri katika ibada ya Ijumaa Kuu, Kanisa la Bikira Maria wa Fatma, lililoko Mwanjelwa mjini Mbeya, Mhashamu Chengula amewashauri waumini wa kanisa hilo kuhakikisha katika jumuiya zao ndogondogo wanajiandaa kumchagua mtu muadilifu kwa kuangalia tabia na mienendo yake badala ya kujikita katika chama anachotoka.

“Imekuwa kawaida kila baada ya uchaguzi mkuu tunaanza kulaumiana. Wakristo wote katika jumuiya zenu ndogo-ndogo nchi nzima muanze kujipanga mnataka mtu wa aina gani, angalieni ana tabia gani na sio anatoka chama gani,” amesema Askofu Chengula.

Alieleza kuwa kwa kufanya hivyo, lawama zinazojitokeza dhidi ya viongozi waliochaguliwa hazitakuwepo.

Aidha, mtumishi huyo wa Mungu alisisitiza kuwa kila Mtanzania ana wajibu wa kuhakikisha nchi inakuwa ya amani na upendo kuanzia jinsi anavyowachagua viongozi na jinsi anavyoishi. Pia, alieleza kuwa ili taifa liendelee kuwa na amani na upendo, uchaguzi wa haki na huru ni muhimu kuzingatiwa.

Aliwataka kuhakikisha kiongozi wanayemchagua hatawafanya waishi kwa kuogopaogopa.

Video: Bombadier aliyofichua Tundu Lissu yaachiwa, Mbowe atuma ujumbe mzito kutoka Gerezani
Parker afunguka alichokiona kwenye macho ya Joshua, kumalizana leo

Comments

comments