Rais wa FC Barcelona Josep Maria Bartomeu amesisitiza suala la kusainiwa kwa mkataba mpya wa mshambuliaji mahiri Lionel Messi kwa kusema hatua hiyo itakamilishwa siku za karibuni.

Hii ni mara ya pili kwa kiongozi huyo kusisitiza jambo hilo, kutokana na tetesi zinazoendelea kuibuka kuhusu mipango ya klabu zilizodhamiria kumsajili Messi kwa dau kubwa.

Bartomeu amelazimika kusisitiza jambo hilo kwa mara nyingine tena, kufuatia maswali mengi ambayo humkabili kila kukicha kutoka kwa waandishi wa habari.

Usiku wa kuamkia hii leo rais huyo alimaliza mzizi wa fitna kwa kuzungumza na kituo cha televisheni cha FC Barcelona na kujibu maswali ambayo yalikua yakikosa majibu ya haraka kuhusu mustakabali wa Messi.

Alisema: Mazungumzo bado yanaendelea na wala hakuna changamoto zozote zilizojitokeza kati yetu na Lionel Messi kama inavyoripotiwa na wanahabari. Alikuja klabuni hapa akiwa na umri wa miaka 13, na leo ana miaka 29, hivyo anajua FC Barcelona ni klabu ya aina gani na ina manufaa gani kwake.

“Najua Messi atapenda kumaliza soka lake akiwa hapa. Tumezungumza nae mara kadhaa kuhusu maisha yake ya sasa na ya baadae na ameonyesha nia ya dhati ya kuendelea kuitumikia FC Barcelona.

“Messi anajua anachokifanya na wakati mwingine huchukua jukumu la kuwahimiza wachezaji wengine kufanya makubwa zaidi kwa ajili ya FC Barcelona, mara zote amekua akifikiria mafanikio.

Dimitri Payet Azigonganisha Arsenal, Man Utd
Victor Lindelof Kumuondoa Smalling Old Trafford