Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa jeshi la polisi linatakiwa kujitathimini utendaji kazi wake ili kuweza kuendana na hali halisi iliyopo kwasasa.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho kwa upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kuna baadhi ya watendaji ndani ya jeshi hilo wanafanyakazi kwa mihemko ya kisiasa.

Mwalimu amesema kuwa kitendo cha jeshi hilo kumkamata mbunge wa Mbeya Mjini kupitia chama hicho, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la ‘Sugu’ akiwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kazi yamesababishwa na mihemuko ya kisiasa.

”Watendaji ndani ya jeshi la polisi wajitathmini, waachane na masuala ya siasa, watalipeleka pabaya taifa, wanatakiwa watimize majukumu yao ya msingi ya kuhakikisha suala la amani na usalama linakuwepo,”amesema Salum Mwalimu.

Hata hivyo, Salum Mwalimu amedai kuwa anachofanyiwa Sugu na jeshi la polisi ni wivu kwasababu anakubalika na kupendwa zaidi na wananchi wa jimbo lake la Mbeya Mjini, hivyo litakuwa jambo jema kama ataachwa afanye kazi yake.

 

Uchakavu wa miundombinu waitesa Maktaba ya Mkoa wa Lindi
TADB yaweka mkakati wa kudhibiti upotevu wa zao la Mahindi

Comments

comments