Serikali nchini India imesema kuwa chanzo cha ajali ya gari moshi iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 300 ni hitilafu katika mfumo wa kielektroniki.

Kwa mujibu wa Televisheni ya New Delhi Waziri anayeshughulikia maswala ya reli nchini India Ashwini Vaishnaw amesema Jumapili kuwa hitilafu hiyo ilisababisha treni kubadili njia kimakosa.

“Nani amefanya hivyo na ni sababu gani itatokana na uchunguzi,” amesema Vaishnaw.

Ufafanuzi huo ulikuja wakati mamlaka ikifanya kazi ya kuondoa mabaki ya treni mbili za abiria ambazo ziliacha njia Ijumaa usiku katika wilaya ya Balasore mashariki mwa jimbo la Odisha, katika moja ya ajali mbaya zaidi za reli katika miongo kadhaa.

Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa ishara ilitolewa kwa treni ya mwendo kasi ya Coromandel Express kuingia kwenye njia kuu ya reli, lakini ishara hiyo ilitolewa baadaye, na badala yake treni ikaingia kwenye laini ya kitanzi iliyo karibu ambapo iligonga treni ya mizigo.

Watu 25 wahofiwa kunywa pombe yenye sumu Songwe
Dkt. Rwezimula: Mabadiliko mtaala wa Elimu kuja na somo jipya