Kiungo mshambuliaji kutoka nchini Algeria Riyad Mahrez na beki wa kati kutoka Ufaransa Aymeric Laporte wamefanyiwa vipimo na kukutwa na virusi vya Corona, kufuatia mchakato uliofanywa na jopo la madaktari la Manchester City, tayari kwa kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya England itakayoanza mwishoni mwa juma hili.

Manchester City wataanza msimu mpya wa Ligi Kuu ya England kwa kucheza dhidi ya Wolves Setemba 21, siku 14 baada ya ligi kuanza

Wawili hao wamebainika kuambukizwa COVID-19, lakini hawaku na dalili zozote kabla, jambo ambalo linaendelea kuzusha hofu kubwa, hasa katika kipindi hiki cha maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kwa ligi ya England.

Klabu ilitoa maelezo yaliyosomeka: “Manchester City imethibitisha kwamba Riyad Mahrez na Aymeric Laporte wamekutwa na COVID-19 baada ya kufanyiwa vipimo.

“Kila mtu anawatakia heri wapone haraka na kurejea mazoezini na kujiandaa na ligi msimu mpya.

Hata hivyo pamekuwepo na ongezeko la visa vya maambukizi ya Corona katika nyanja ya michezo ulimwenguni kote kwa siku za hivi karibuni.

Beki wa kati kutoka Ufaransa Aymeric Laporte

Mabingwa wa Ufaransa (Ligue 1) Paris Saint-Germain ambao wanatarajia kuanza kucheza mashindano ya ndani siku ya Al-khamisi wameripoti visa sita vya maambukizi kati ya wachezaji wao katika kikosi.

Mchezo wa kwanza wa Ligue 1 ulihairishwa mwezi uliopita baada ya Marseille kuthibitisha kuna wachezaji wawili ndani ya kikosi wamepata Corona.

Paul Pogba, Houssem Aouar na Steve Mandanda nao walishindwa kujiunga na timu ya Ufaransa katika michuano ya Nations League baada ya kuambukizwa Corona.

Balozi apongeza usimamizi wa sheria ya usalama kazini
Bwawa la Nyerere kuzalisha umeme megawati 2115