Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limekusanya Sh. bilioni sita za tozo ya kivuko kwa miezi nane, katika daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam.
NSSF inakuwa taasisi ya pili ndani ya wiki moja kutangaza mapato ya mradi, baada ya mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (Dart) kufanya hivyo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara,amesema kuwa mradi wa daraja hilo umeingiza jumla ya sh. bilioni  sita kuanzia mwezi Mei 2016, hadi januari 2017,ikiwa ni juu ya lengo kwa asilimia 20.
Aidha, Prof. Kahyarara amesema gharama za uendeshaji wa daraja hilo katika kipindi hicho ni jumla ya Sh. milioni 800 tu na kuongeza kuwa  NSSF imemudu kuvuka lengo kwa wastani wa asilimia 20 kutokana na kutumia waajiriwa wake badala ya wakala.
“Tunaziwekeza moja kwa moja BoT, Benki Kuu katika mnada wa dhamana za Serikali (treasury bonds) ambayo ni ya asilimia 13.5 ambayo ikiiva miaka 15 ijayo ni Sh. bilioni 18. utaratibu huu tumeona unalifanya Shirika kuwa na uhakika, kwamba likihitaji fedha ya haraka wanaweza kuzitumia na taarifa zitaonyesha fedha za daraja zilishapatikana,ni ubunifu tulioanzisha kwa kuwa tuliona ukiweka sekta binafsi huwezi kupata faida hiyo,” amesema Kahyarara.
Hata hivyo, Prof. Kahyarara amebainisha kuwa NSSF ilitaka tangu siku ya kwanza ya kutumika kwa daraja hilo faida ianze kukusanywa jambo ambalo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Daraja hilo lilizinduliwa Aprili 19, mwaka jana, na Rais John Magufuli na lina urefu wa mita 680 na jumla ya barabara sita.

Liverpool Wamvutia Kasi Adam David Lallana
Jackson Martinez Atamani Kurudi Ulaya