Mama mmoja amesababisha kifo cha mtoto wake mmoja na kuwaacha wanne mahututi baada ya kuwanywesha dawa ya kienyeji, watoto hao wa familia moja wamenyweshwa dawa hiyo mkoani Kigoma wilaya ya Buhingwe.

Manusura wanne walikimbizwa kituo cha afya Muyama na baadae wakapelekwa hospitali ya wilaya ya Kasulu Mlimani kwa matibabu zaidi.

Aidha, Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya cha Muyama, Joackim Kulwa Muhaya amesema kuwa mtoto mmoja amefariki nyumbani na wao walipokea watoto wanne wakiwa wamevimba tumbo na macho ya njano, na kutokana na hali hiyo waliwafanyia vipimo na kugundua walipewa dawa ya kienyeji.

“Hali za watoto hao zilikuwa mbaya sana, tuliwapa huduma ya kwanza na kwakuwa hatukuwa na vipimo vya kuangalia utendaji kazi wa ini na figo ilibidi kuwapa rufaa waende Hospitali ya wilaya ya Kasulu Mlimani kwa huduma zaidi” amesema Mganga Joackim.

Muhaya ametoa wito kwa jamii kuwa makini na matumizi ya dawa za kienyeji kwasababu hazina vipimo maalum,na zipo tofauti na za Hospitali ambazo mgonjwa anapewa kutokana naugonjwa unao msumbua pamoja na kuzingatia umri.

Kwa upande wake shangazi wa watoto hao ambaye ana wauguza hospitali amesema kuwa yeye alikuwa kwenye shughuli zake ndipo walipokuja watu watatu na kumjulisha kuwa watoto wa kaka yake hali zao ni mbaya sana na mmoja kafariki.

Naye Diwani wa kata ya Kajana, Rabson Ngeze amesema kuwa mama huyo alikuwa na mgogoro na mume wake na dawa hiyo aliwapa watoto ili wamsahau baba yao na badala yake ikageuka sumu, pia mama huyo alitoweka pasipojulikana baada ya kufanya tukio hilo na wanakijiji wana msaka kila kona.

Sadio Mane aimarisha ndoa Anfield
Nicklas Bendtner kutumikia kifungo

Comments

comments