Wanafunzi wawili wa kike wa darasa la 8 katika shule ya msingi Kizingitini huko Lamu Kenya wanashikiliwa na polisi kwa kufanyiana vurugu shuleni na kukatana mapanga baada ya kumgombania mwanaume.

Taarifa ya kituo cha habari cha Citizen Kenya Inasema ugomvi wa waili hao ulianzia darasani baada ya mmoja wao kumshutumu mwenzake kuwa na mahusiano na DJ huyo ambae na yeye pia alikua akimpenda.

Inasemekana baada ya mmoja huyo kumvamia mwenzake alimkata na jembe usoni na mwingine akatoa kisu na kumchoma mwenzake mkononi.

Wawili hao mpaka sasa wanashikiliwa na kituo cha polisi cha Kizingani ambapo bado wananedlea na matibabu ya vidonda vyao.

Hata hivyo insemekana Mwanaume huyo DJ amejificha wakati polisi wakiendelea kutafuta chanzo cha wawili hao kugombana.

Rais Samia ahimiza ufugaji wa kisasa
Mfanyakazi wa ndani ahukumiwa kifungo jela kwa kumdhalilisha kijinsia mtoto anaemlea.