Aliyewahi kuwa meneja wa klabu ya Ajax Amsterdam David Endt amepokea kwa mshtuko taarifa za kutimuliwa kwa Frank de Boer baada ya siku 85 za kuanza kwa ajira yake Inter Milan.

Endt amesema pamoja na kufahamu changamoto zilizokua zikimkabili De Boer tangu alipoanza msimu huu katika ligi ya nchini Italia, bado hakudhani kama uongozi wa Inter Milan ungeweza kufikia hatua ya kumngufulia mlango na kumtimua.

Amesema aliamini ni mapema mno kwa viongozi wa klabu hiyo ya San Siro kumtimua De Boer kutokana na ugeni wake katika ligi ya nchini Italia, jambo ambalo limekua kinyume na matarajio yake.

“Inter Milan wanaonekana wazuri wakiwa katika mavazi yao ya rangi ya bluu na nyeusi, lakini kwa kitendo walichokifanya hawana tofauti na mwanamke kahaba,” Alisema Endt alipohojiwa na vyombo vya habari vya Uholanzi.

“Tangu mwanzo niliona kuna viashiria kwa Frank de Boer kushindwa kufanya majukumu yake ipasavyo, kwa sababu ya falsala za kidachi alizokua anazitumia, Inter Milan walipaswa kuheshimu hilo.

“Niliwahi kuzungumza na Frank na nilimkanya kuhusu maamuzi ya kujiunga na klabu ya Inter Milan lakini alinipuuza, na sasa ameona matokeo yake. Kwa bahati mbaya ameondoka kwa kudhalilika.

“Nakumbuka nilimsihi asifanye maamuzi magumu ya kwenda katika nchi ambayo haina mfumo wa soka kama la Uholanzi, na nilimuhakikishia kwa kumwambia ukweli wa mambo, kwa sababu nilijua Inter Milan walihitaji nini katika kipindi hiki,

“Inter wamekua na jina kubwa katika ramani ya soka duniani na walitamba sana miaka ya nyuma, lakini kwa sasa wanashindwa kujielewa kutokana na kuamini bado wana uwezo wa kisoka kwa kutamani mafanikio ya haraka, wanashindwa kutambua changamoto iliyo mbele yao ni kujipa muda wa kujitengenezea njia ya kurudi katika mafanikio.

“Frank aliaminiwa sana na viongozi wa Inter Milan, na wengi wao walidhani angeweza kufanya mabadiliko kwa haraka kama walivyotarajia, lakini wameona mambo yanachelewa na mwishiwe wamemtimua.

“ilikua ni vugumu kwake kufikia malengo, kwa sababu hakufanya maandalizi ya kikosi, na badala yake kazi hiyo ilianzishwa na Roberto Mancini, ambaye siku chache kabla ya kuingia katika ligi aliondoka.” Alisema Endt

Mwamuzi Wa Kike Tanzania Kuchezesha Afcon Ya Kinamama
Mahakama yamtia hatiani Lady Jay Dee dhidi ya Ruge, Kusaga