Meneja wa klabu ya Newcastle United Rafa Benitez ameadhibiwa kwa kutozwa faini ya Pauni 60,000, kufuatia kosa la kumtuhumu mwamuzi  Andre Marriner kabla ya mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England uliowakutanisha dhidi ya Crystal Palace kwenye uwanja wa Selhurst Park,  Septemba 22.

Chama cha soka nchini England (FA) kilimfungulia mashataka meneja huyo kutoka nchini Hispania siku moja baada ya kutoa kauli ya kutokua na imani na mwamuzi huyo, kwa kukumbushia aliyowahi kuyafanya dhidi ya wachezaji wake.

Kabla ya FA kutoa hukumu, Benitez aliwasisha utetezi wake ambao ulieleza kuwa: “Nina imani kubwa na mwamuzi Andre Marriner, na nilichokizungumza kabla ya mchezo dhidi ya Crystal Palace, hakikua na maana ya kumtuhumu ama kumkashifu, nilijaribu kuzungumzia michezo iliyopita.”

Kwangu ni mwamuzi mwenye uzoefu mkubwa ambaye anaweza kuwa na mapungufu kama waamuzi wengine, niliamini kusema kule kungeweza kuwawezesha mashabiki kutambua ni vipi nilivyowahi kuumizwa na hatua ya kuwaonyesha kadi wachezaji wangu, msimu uliopita.

Hatua ya kutozwa faini ya Pauni 60,000 itamfanya Benitez kupoteza kiasi hicho, kwenye mshahara wake wa Pauni 330,000 anaopokea kwa mwezi.

Mchezo kati ya Newcastle Utd na Crystal Palace ulimalizika kwa klabu hizo kugawana alama moja, moja, kufuatia sare ya bila kufungana iliyopatikana ndani ya dakika 90.

Hatma ya De Bruyne mikono mwa madaktari
Video: Kauli ya Bashiru yagonga vichwa, Waliokusanya kodi 'kiduchu' matatani

Comments

comments