Beki na nahodha wa klabu ya Southampton Jose Fonte amewasilisha barua ya kuomba aondoke klabuni hapo.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 33, amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja na nusu, ambao aliusaini mwezi Oktoba mwaka 2015.

Mkurugezi wa soka wa Southampton Les Reed, amesema Fonte alikua na nafasi ya kuendelea kubaki klabuni hapo kwa kusainishwa mkataba mpya, lakini kutokana na ombi lake hawana budi kuheshimu alichokidhamiria.

“Amekua na bahati mara kwa mara ya kucheza soka lake hapa, na tulikua na mpango wa kuendelea kuwa nae kwa kipindi kingine.” Reed aliiambia BBC Radio Solent.

“Amekua muwazi na tumependezwa na jambo hilo, na kwa upande wetu hatutokua na hiyana ya kulikataa ombi lake ambalo lipo mezani kwa sasa.

Hata hivyo Reed amesema mpaka sasa hakuna ofa yoyote iliyowasilishwa klabuni hapo kwa ajili ya usajili wa Fonte katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili, hivyo wataendelea kusubiri na kuona ni wapi ambapo wataonyesha nia ya kumuondoa St Marries Stadium.

Fonte alijiunga na klabu ya Southampton mwaka 2010, akitokea Crystal Palace, na mpaka sasa ameshaitumikia The Saint katika michezo 288.

Majaliwa atoa onyo kwa Madiwani na watumishi
Marco Silva Akubali Kubeba Mzigo