Msanii wa kizazi kipya Gift, maarufu kama Gigy Money amefunguka na kusema wasichana wapunguze kuimba maneno magumu na kutumia vingereza lugha ambazo hazieleweki na watu wote katika muziki kunawafelisha ndio maana inawawia vigumu muziki wao kuwafikia watu wa rika lote.

Gigy alizungumza hayo wakati akitoa ufafanuzi juu ya wimbo wake mpya unaofanya vizuri unaoenda kwa jina la Papa.

“Nitoe ushauri kwa wasichana ambao wanaimba, unajua wasichana wengi wana vipaji vya kuimba lakini wanafeli.  Ukishajijua huwezi kuimba acha kuimba vitu vingi, huna uwezo wa kuimba alafu mambo unayoimba mlolongo kibao, vingereza, sijui nini utajikuta unafeli. Sasa neno kama ‘papa’ lipo uswahilini, rahisi kwa watu kuelewa”, amesema Gigy Money.

Gigy ameeleza kuwa lengo lakutoa wimbo huo wenye lugha nyepesi ilikuwa ni kuwafikia watu wenye rika lote, na anaamini kwa asilimia kubwa amefanikiwa.

 

Mlinda mlango Goran Lenac apigwa risasi
Video: Diamond afunguka kuhusu mtoto wa Hamisa Mobeto