Meneja wa Man City Pep Guardiola anakaribia kustaafu kufundisha soka licha ya kutangaza huenda angefanya hivyo atakapofikisha umri wa miaka 65.

Meneja huyo kutoka nchini Hispania amewahi kuifundisha klabu ya Barcelona kwa mafanikio makubwa kisha Bayern Munich kabla ya kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrini huko Etihad Stadium.

”Nitakuwa hapa Manchester kwa misimu ama mitatu labda na zaidi,” Guardiola mwenye miaka 45 alisema kabla ya ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Burnley.

”Sitakaa kwenye benchi mpaka miaka 60-65.Nafikiri mchakato wa kuanza kusema kwaheri umekaribia.

Guardiola ameshinda vikombe 14 katika miaka minne akiwa na Barcelona, ikiwa ni pamoja na mataji matatu ya La Liga na mawili ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Alipumzika mwaka mzima kabla ya kujiunga na Bayern Munich na kuwaongoza kupata mataji matatu ya ligi kuu.

Katika mchezo wa jana dhidi ya Burnley, kikosi cha Guardiola kilicheza pungufu baada ya Fernandinho kupewa kadi nyekundu lakini mabao ya Gael Clichy na Sergio Aguero yaliwapa ushindi.

Kocha Wa Ivory Coast Amnyima Raha Jose Mourinho
Bilic Amtuhumu Mwamuzi, Adai Man Utd Wamebebwa