Bingwa mara tatu wa dunia wa ngumi za uzito wa juu , Mohammad Ali amefariki akiwa na umri wa miaka 74 nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bob Gunnell ambaye ni msemaji wa familia, Mohammad Ali amefariki jana usiku katika hospitali ya Phoenix alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa akipatiwa matibabu .

Mohammad Ali amefariki baada ya kupambana kwa zaidi ya miaka 30na ugonjwa unaofahamika kama Parkinson ambao ulipelekea kuwa anatetemeka sehemu kadhaa za mwili hususan kichwani na mikononi.

Bondia huyo anayetajwa kuwa ‘Bondi Bora wa Muda Wote’ (The Greatest of All Time) anatarajiwa kuzikwa katika mji wa Louisville, Kentucky ambako alizaliwa.

 

Kange Lugola: Wasaidizi wa Rais wamempotosha kuhusu wanafunzi wa UDOM
CAF Yatoa Haki Za Matangazo Kwa Azam TV