Beki wa kati Hassan Isihaka amejiunga na klabu ya Ndanda FC, akitokea kwa Wekundu Wa Msimbazi Simba, ambapo amedumu tangu akiwa na kikosi cha vijana cha klabu hiyo kongwe hapa nchini.

Isihaka anaondoka Msimbazi, huku akiacha kumbukumbu ya kusimamishwa kwa mwezi mmoja na kuvuliwa unahodha kwa madai ya kumjibu kwa lugha isiyo ya kiungwana kocha wake, Jackson Mayanja baada ya kumjumuisha kwenye kikosi kilichopambana na Singida United katika mchezo wa kombe la FA.

Isihaka alimuuliza Mayanja ‘Kwa nini haukunichezesha dhidi ya Yanga na umenipanga katika mchezo dhidi ya Singida?’

Yalikuwa ni makosa ambayo hakuna aliyekuwa upande wake na aliporejea hakuwa mchezaji muhimu tena, kwani nafasi yake ilichukuliwa na beki mwingine aliyeaminiwa na Mayanja, Novatus Lufunga ambaye alicheza karibu michezo yote kabla ya msimu wa 2015-16 kufikia tamati mwezi Mey mwaka huu.

Ishihaka amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu ya Ndanda FC ya mkoani Mtwara, na anaaminika huenda akaleta changamoto mpya katika safu ya ulinzi ya klabu hiyo kuanzia msimu wa 2016-17 ambao umepangwa kuanza Ogasti 20.

Serikali Kukarabati kwa Kasi Shule Iliyoungua Moto
Picha: Theresa May alivyokabidhiwa rasmi Uwaziri Mkuu Uingereza, ampigia goti Malkia