Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa kesho Julai 2, 2021 anatarajiwa kufunga Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Sekondari (UMISSETA) kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Mashindani hayo yenye kauli mbiu “Michezo, Sanaa na Taaluma kwa Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda, yalianza majuma mawili yaliyopita kwa kupewa baraka na Waziri Mkuu Kaqssim Majaliwa.

Mashindano ambayo hushirikisha timu za shule za Sekondari kwa michezo yote yamejumuisha mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wadau mbalimbali kama vile vyama vya michezo, mashirikisho na vilabu vya michezo mbalimbali vilialikwa kuja kuangalia vipaji mbalimbali.

Viwanja vilivyotumika katika UMISSETA ni pamoja na viwanja vya Nangwanda Sijaona, Chuo cha Walimu Mtwara (TTC kawaida) Chuo cha Walimu Ufundi maarufu kama Mwasandube, na viwanja vya Shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara.

Michezo iliyoshindaniwa katika mashindano haya ni mpira wa miguu kwa wasichana na wavulana, mpira wa miguu maalum kwa wavulana (wenye ulemavu wa kusikia) mpira wa pete, mpira wa wavu kwa wasichana na wavulana, mpira wa mikono kwa wasichana na wavulana, mpira wa kikapu kwa wasichana na wavulana, mpira wa meza kwa wasichana na wavulana, riadha jumuishi, kwaya na ngoma.

Aidha mashindano ya mwaka huu yamekuwa na hamasa kubwa kwa kuwa yatapambwa na wasanii wa kizazi kipya ili kutoa hamasa na burudani. baadhi ya wasanii ambao watapanda jukwaani kesho ni pamoja na Maarifa, Kala Jeremiah,GNacko,Mr.Blue, Shishi, Nandy na Sholo Mwamba.

Manara amkubali mzee Mpili, kumpa milioni moja
KMC FC kuikabili Simba SC kwa Mkapa