Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, amesema kuwa jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha linatokomeza uhalifu na kutenda haki wakati wa kutekeleza majukumu yao ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Mwanza wakati wa muendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha katika mikoa mbalimbali nchini, ambapo amesema kuwa jeshi hilo limejipanga kikamilifu kuhakikisha hali ya usalama inakuwa shwari.

Aidha, IGP Sirro, ametoa wito kwa wananchi na raia wema kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuweza kudhibiti vitisho mbalimbali ya uhalifu yanayoweza kujitokeza katika maeneo yao.

Hata hivyo, Sirro amefanya mazungumza na askari wa Jeshi la polisi mkoani Mwanza ikiwa ni pamoja na kujitambulisha kwenye kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo ambapo amesisitiza weledi wakati wa utekelezaji wa majukumu.

Lissu arudishwa rumande, tarehe ya hatma ya dhamana yake yatajwa
Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu yazinduliwa