Baada ya kupata suluhu dhidi ya Simba, Klabu ya Azam imejinasibu kuwa kikosi chao kipo vizuri tofauti na watu walivyokuwa wakikibeza kikosi chao kabla ya msimu huu kuanza.

Afisa Habari wa Azam FC, Jaffar Iddy amezungumza juu ya hilo kwa kusema kuwa matokeo ya suluhu dhidi ya Simba, Jumamosi iliyopita huku Azam ikionyesha kiwango kizuri na kuipa Simba wakati mgumu yametibitisha ubora wa kikosi chao.

Akizungumza zaidi, Jaffar alisema: “Mchezo wetu na Simba umewaumbua wote waliokuwa wakisema tumesajili watoto na hatutaweza ushindani, hoja hiyo ilikuja baada ya baadhi ya wachezaji wetu wachache kuondoka na kwenda kujiunga katika timu nyingine, hiyo inamaanisha kuwa tuna kikosi kizuri tofauti na ilivyokuwa ikidaiwa na baadhi ya watu.

Marekani itajuta kama itaendelea kutuchokoza: Korea Kaskazini
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Septemba 13, 2017