Ofisi ya Msajili ya Vyama vya Siasa imesema Profesa Lipumba bado ni Mwenyekiti wa halali wa Chama cha Wananchi (CUF) kwa sababu alitengua barua yake ya kujiuzulu kabla haijakubaliwa na mamlaka yake ya uteuzi kama inavyoelekeza ibara ya 117(2).

Ufafanuzi huo umetolewa na Sisty Nyahoza kwa niaba ya Msajili wa Msajili wa Vyama vya Siasa leo Septemba 26, 2016 ambapo ameeleza kwamba msimamo alioutoa Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu mgogoro wa uongozi katika chama cha CUF una maana kwamba kwa mujibu wa Katiba ya CUF toleo la 2014, Prof. Lipimba bado ni Mwenyekiti halali wa chama hicho.

Ufafanuzi huo ni kufuatia taarifa zinazoenezwa na vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa amesema kuwa hakumrudishia Prof. Lipumba Uenyekiti wa Taifa wa CUF, bali kajirudisha mwenyewe kinyemela, Hivyo Ofisi ya Usajili imesema habari hiyo siyo za kweli, imepotoshwa kwa makusudi na Watanzania wanapaswa kuipuuza.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imewaasa viongozi wa kitaifa wa CUF, kusoma kwa makini msimamo uliotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasana kuuheshimu kwani kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258, Msajili anawajibu wa kujiridhisha kwamba, mabadiliko yoyote yaliyofanywa katika uongozi wa taifa wa chama cha siasa ni halali na yanaheshimiwa na mamlaka halali kwa mujibu wa Katiba ya chama husika.

Trump, Clinton washambuliana kuhusu vita Iraq, Trump abanwa na kodi
Majaliwa awasili Kibiti wilayani Kilwa kwa ziara ya kikazi