Tiketi za mchezo wa watani wa jadi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC Jumamosi, Februari 20, 2016 zimeanza kuuzwa leo Ijumaa saa 2 asubuhi leo asubuhi katika vituo 10 mbalimbali vilivyopo jijini Dar es salaam.

Vituo vinavyotumika kuuza tiketi za mchezo huo ni ofisi za TFF – Karume, Buguruni Oilcom, Ubungo Oilcom, Uwanja wa Taifa Temeke, Mavuno House – Posta, Dar Live Mbagala, Breakpoint – Kinondoni, Kidongo Chekundu – Mnazi Mmmoja, Mwenge na Kivukoni Ferry.

Kiingilio cha juu cha mchezo huo ni shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa VIP A, Elfu Ishirini (20,000) VIP B & C, Elfu Kumi (10,000) kwa viti vya rangi ya machungwa (Orange), na Elfu Saba (7,000) kwa viti vya rangi ya bluu na kijani.

Milango ya Uwanja wa Taifa itafunguliwa kuanzia saa 5 kamili asubuhi, huku barabara ya Chang,ombe ikifungwa kuanzia asubuhi, na magari maalumu yenye stika maalumu ndiyo yatakayoruhushiwa kuingia eneo la uwanja wa Taifa kwa kupitia barabara ya Mandela na uwanja wa Uhuru.

Upande wa ulinzi, Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama watakuwepo kuhakikisha usalama wa wapenzi wa mpira watakaokuja kushuhudi mchezo huo, vitu kama silaha, vilevi, mabegi na vitu vyenye ncha havitaruhusiwa kuingia ndani ya uwanja.

Shirikisho linawaomba wapenzi, wadau na washabiki wa mpira wa miguu nchini kununua tiketi katika magari ya kuuzia tiketi katika vituo vilivyotajwa, ili kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi zisizo halali kwa mchezo huo.

Mchezo huo utachezeshwa na mwaamuzi Jonesia Rukyaa (Kagera), akisaidiwa na mwamuzi Josephat Bulali (Tanga), Samwel Mpenzu (Arusha) wote wakiwa wakiwa waaamuzi wenye beji za FIFA, mwamuzi wa akiba Elly Sasii (Dar) na Kamisaa wa mchezo huo atakua Khalid Bitebo (Mwanza).

Jamal Malinzi Asambaza Ujumbe Wa Kupanga Matokeo
Papa Francis, Donald Trump wavutana kuhusu ukristo wa Mgombea huyo