Mtu mmoja ambaye Jina lake kimehifadhiwa mkazi wa Jijini Dar es salaam anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro baada ya kukutwa akitumia jina la Waziri wa zamani, William Lukuvi kuendesha mafunzo ya ujasiriamali mkoani humo na kujipatia zaidi ya Sh milioni 2.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Simon Maigwa amesema alikuwa akijipatia Sh. 35,000/= kwa kila mshiriki wa mafunzo hayo huku akiwaahidi kuwalipia kila mmoja Sh300,000 kama ada baada ya kuhitimu mafunzo hayo na kwamba kuwapatia ajira.

“Baada ya kupata taarifa hizi jeshi la polisi tulifanya njia mbalimbali na kumkamata akiwa katikati ya Mafunzo na tuliwasiliana na viongozi ambao mtuhumiwa huyu alikuwa akiwataja ambapo walimkana na kwamba hawamjui, hivyo tunaendelea kumshikilia kwa hatua zaidi,” amesema Kamanda Maigwa.

Mtuhumiwa huyo amekuwa akiendesha mafunzo hayo ya ujasiriamali katika mikoa mbalimbali ya Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Arusha, Mbeya na Tanga kwa kujipatia kipato isivyo halali.

Pikipiki yauwa Watanzania watatu Kenya
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 17, 2022