Jose Mourinho ameibua jambo katika baadhi ya vyombo vya habari, kufuatia nia yake ya kutaka kumsajili kiungo kutoka nchini Wales na klabu ya Arsenal, Aaron Ramsey.

Gazeti la The Sun limekua la kwanza kuripoti taarifa hiyo ambayo imeshtua umma wa wapenda soka duniani, kutokana na upinzani uliopo kati ya Arsenal na Man Utd.

Hata hivyo taarifa hizo zinadai kwamba, mpango wa Jose Mourinho wa kutaka kumsajili Ramsey umeibuka kutokana na shabaha ya kumuhamisha kiungo wa klabu ya Borussia Dortmund, Henrikh Mkhitaryan kuelekea Old Trafford kuonyesha dalili za kugonga mwamba, kufuatia mkataba uliopo.

Mourinho anaamini Ramsey ana vigezo vya kuwa kiungo mashuhuri, kama alivyoweza kufanya kazi na Frank Lampard kwenye klabu ya Chelsea.

Thamani ya Ramsey mwenye umri wa miaka 25, inakadiriwa kufikia Pauni million 50, kwa mujibu wa mkataba wake na Arsenal, lakini tayari imeshaonyesha dhahir maafisa wa Emirates Stadium, hawako tayari kumuachia kuondoka.

Mzamilu Yasin Amtumia Salam Jonas Mkude
Pam D: Sibebwi na Midundo ya Mesen