Kesi maarufu ya uchuguzi mkuu mwaka huu ya kutaka tafsiri ya sheria kuhusu kukaa au kutokaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura baada ya kupiga kura, inatarajiwa kukatiwa rufaa baada ya Mahakama Kuu kutoa uamuzi wa kutokaa katika eneo hilo baada ya kupiga kura.

Ammy Kibatala, aliyepeleka kesi hiyo mahakamani pamoja na Wakili wake Peter Kibatala, wameeleza kuwa wanaheshimu maamuzi ya mahakama hiyo lakini bado hawajaridhishwa na maamuzi hayo hivyo wamepanga kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa.

“Siwezi kusema nimekubaliana na uamuzi wa Mahakama na ndio maana nasema tunataka tukate rufaa, na nimeshauriana na wakili wangu tutakata rufaa. Sijakubaliana na uamuzi huo kwa sababu ile kiu yetu ya kutaka kujua tafsiri halisi ya kile kifungu haijakatwa bado,” alisema Ummy Kibatala.

Hata hivyo, Bi. Kibatala alieleza kuwa rufaa hiyo itasikilizwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu bali itasaidia katika chaguzi zijazo kwa kuwa kesho ndio siku ambayo watanzania watapiga kura katika Uchaguzi Mkuu.

 

Kikwete: Magufuli Anasubiri Kuapishwa Tu
Pape N’daw: Ninasingiziwa, Sikuvaa Hirizi