Serikali imepanga kuanzisha mahakama katika maeneo ya viwanja vya ndege na bandarini ili kuendesha haraka kesi za watuhumiwa wanaokutwa na dawa hizo katika maeneo hayo.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde ameweka wazi mpango huo leo bungeni alipokuwa akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.

Alisema kuwa tayari Serikali imeanza kufanya mazungumzo na wadau wa ikiwemo mahakama kuhusu mpango huo.

“Serikali imeshaanza mazungumzo ya awali na wadau wa haki jinai ikiwa ni pamoja na mahakama ili kuona uwezekano wa kusikiliza mashauri mapema mara mtuhumiwa anapokamatwa,” alisema Mavunde alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chadema, Grace Tendega.

Naibu Waziri huyo alisema kuwa hatua hiyo inafanywa kwa kufuata mfano wan chi mbalimbali zinazokabiliana na usafirishaji wa dawa za kulevya kama India.

Hivi karibuni, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema kuwa Serikali imepiga hatua kubwa katika kupambana na biashara ya dawa za kulevya.

Moto wateketeza soko,15 wafariki dunia
Video: Baada ya kunusurika kifo, Mnangagwa, JPM uso kwa uso, Hoja za wabunge zaipa tabu Serikali