Wachezaji Kibwana Shomari na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ wamoendoka nchini Tanzania na kuelekea Tunisia kwa ajili ya kufanyiwa matibabu kutokana na majeraha yanayowakabili.

Taarifa kutoka Young Africans zinaeleza kuwa, wachezaji hao wameambatana na daktari wa viungo Youssef Mohamed, ambaye atakua nao nchini Tunia wakati wote wa matibabu yao.

Kibwana na Ninja wamekosekana kwenye michezo kadhaa ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ pamoja na Kombe la Mapinduzi.

Kibwana, ambaye anacheza beki ya kulia na kushoto, ndiye anayeonekana kukosekana kwake kumekuwa pengo kwenye klabu hiyo na kuonekana hata kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kiasi cha kuvuliwa ubingwa.

Wachezaji hao wanafikisha idadi ya wachezaji watatu wa Young Africans kupelekewa Tunisia kwa matibabu. Mwezi Novemba mwaka jana (2021), Young Africans ilimpeleka nchini humo Mshambuliaji kutoka Burkina Faso, Yacouba Songne na kufanyiwa upasuaji wa goti. Kwa sasa mchezaji huyo anauguza jeraha, ambalo kwa mujibu wa madaktari anatakiwa kukaa nje miezi mitano ili aanze tena mazoezi mepesi.

Shiboub, Moukoro OUT Simba SC
Abdhamid Moallin: Ninaifahamu Simba SC