Mkurugenzi wa kituo cha kulea watoto, Stephen Nzuki Mutisya (29), amehukumiwa kifungo cha karne moja, (miaka 100)

Mutisya, ambaye raia wa Kenya amehukumiwa kifungo hicho kufuatia kupatikana na hatia ya kunajisi wavulana wenye umri mdogo.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Milimani, Zainab Abdul amesema ametoa hukumu hiyo kwani kitendo alichokifanya Mutisya ni cha kinyama.

Amesema wavulana na wasichana wadogo ambao hawana nguvu za kujitetea wanahitaji kulindwa kikamilifu na jamii na kamwe Mahakama haitavumilia vitendo vya namna hiyo.

Stephen Nzuki Mutisya, amepatikana na kifungo hicho baada ya Mahakama kujiridhisha kuwa alinajisi wavulana hao katika nyumba ya watoto iliyopo mtaa wa Utawala jijini Nairobi nchini Kenya, kati ya 2010 na 2016.

Bwege kumnadi Raila Odinga
MCT yatoa tathmini uhuru wa vyombo vya Habari nchini