Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Francis Baraza amejivunia kuwa Kocha aliyemnoa Kiungo kutoka Tanzania Novatus Dismas, ambaye kwa sasa anacheza soka la Kulipwa nchini Ubelgiji katika Klabu ya Zulte Waregem.

Kocha huyo kutoka nchini Kenya alifanya kazi ya kumnoa kijana huyo wakati akiwa Mkuu wa Benchi la Ufundi la Biashara United Mara, ilipokua ikishiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha Baraza amesema: “Najivunia Novatus Dismas kwa sababu wakati nilimkuta Biashara United akiwa kwa mkopo akitokea Azam FC. Chini yangu alicheza mechi zote za Ligi Kuu”

“Mwisho wa msimu akatangazwa mchezaji bora kijana, akaitwa timu ya Taifa pamoja na Daniel Mgore na Abdulmajid Mangalo”

“Kuna wakati Novatus alikuwa anaenda njia mbaya, nikamuita na kuzungumzanae kama mzazi. Nilimwambia ana uwezo mkubwa sana na muda si mrefu atapata timu nje ya nchi”

“Nikamwambia aachane na kundi fulani halafu aweke bidii kwenye mazoezi. Jambo zuri alinielewa akabadilika akawa anajituma sana mazoezini.Kwa hiyo hata alivyoondoka kwenda Macabbi telaviv haikuwa kwa bahati”

“Kuna kijana wangu [Joseph Okumu] nilimshika mkono kutoka shule [alikuwa anasoma Sekondari] nikamchukua kwenye timu yangu sasa hivi anacheza Gent, Belgium.”

“Nimemwambia amtafute Novatus Dismas akaenae wazungumze kwa ajili ya kumjenga kwa sababu bado ni kijana mdogo.”

Masau Bwire aitambia Young Africans
Waliopona Ebola marufuku tendo la Ndoa