Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka nchini Malawi Nyasa Big Bullets Kalisto Pasuwa amewaomba radhi Mashabiki wa klabu hiyo baada ya timu yao kutolewa mapema kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Nyasa Big Bullet ilitupwa nje ya Michuano hiyo mwishoni mwa juma lililopita (Jumapili-Septemba18), kwa kupoteza mchezo wa Mkondo wa Pili kwa 2-0, na kuifanya timu hiyo kupoteza kwa matokeo ya jumla 4-0, dhidi ya Simba SC ya Tanzania.

Pasuwa amesema licha Nyasa Big Bullets kutawala soka la Malawi lakini imeshindwa kusonga mbele katika Michuano ya Klabu Bingwa Afrika, halia mbayo imemfedhehesha sana katika soka la nchini humo.

Amesema Mipango ya klabu hiyo yenye mashabiki wengi nchini Malawi ilikua ni kutinga hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, lakini imekua tofauti, hivyo hawana budi kukubaliana na matokeo, na kuangalia mbele katika Michuano ya ndani wanayoendelea kushiriki.

“Tumeshindwa kuendelea na mashindani wa Afrika, halikua lengo letu kuishia hapa, tulijipanga kufanya makubwa zaidi ya hapa, ila imekua bahati mbaya sana kwa Nyasa Big Bullet.”

“Kwa niaba ya Wachezaji wangu ninawaomba radhi Mashabiki wote wa Nyasa Big Bullet kwa kushindwa kufikia lengo la kupambana kimataifa, tumekua na matokeo mazuri hapa Malawi kwa kipinid kirefu, kutolewa kwenye Mashindano ya Afrika kumetutia doa kubwa.” amesema Kocha huyo kutoka nchini Zimbabwe

Kikosi cha Nyasa Big Bullet leo Ijumaa (Septemba 23) kinacheza mchezo wa Nusu Fainali FDH Bank Cup dhidi ya Mukuru Wanderers FC katika uwanja wa kimataifa wa Bingu, mjini Lilongwe.

Mshindi wa mchezo huo atacheza Fainali dhidi ya Bullets Reserves Oktoba 8.

Wabunge EALA watakiwa kuliwakilisha vyema Taifa
Kennedy Juma: Kocha Mgunda ananiamini