Klabu ya Leicester City imethibitisha kuwa itakata rufaa mbele ya FA kupinga kadi nyekundu aliyozawadiwa mchezaji wake Jamie Vardy katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stoke City, Jumamosi iliyopita.

Vardy aliopigwa kadi nyekundi kiutata na mwamuzi Craig Pawson katika dakika ya 28 ya mchezo huo uliomalizika kwa sare ya 2-2, baada ya kukumbana na Mame Biram Diouf.

Hata hivyo, Bosi wa Stoke, Mark Hughes ameonesha kushangazwa na uamuzi wa Leicester akidai kuwa uhalali wa kadi ile nyekundu uko wazi na haoni sababu ya timu hiyo kulalama.

Alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Kocha Claudio Ranieri kulalama muda mfupi baada ya mtanange huo kukamilika, akipingana kwa nguvu na uamuzi huo huku akiweka wazi mpango wa kukata rufaa ambao sasa umethibitishwa.

“Klabu imefungua shtaka kuhusu hatua ya kuondolewa mchezoni kimakosa na tunatarajia kusikia matokeo ya rufaa katika siku chache zijazo,” imeeleza sehemu ya tamko la Leicester ambao ni mabingwa wa Uingereza.

Vardy aling’olewa mchezoni kwa kadi nyekundu kabla timu zote hazijapata goli lakini baadae Stoke walikukuruka na kupiga magoli mawili kabla ya mapumziko.

Lakini Leicester ililipa kipigo hicho kwa magoli ya baadae sana kutoka kwa Leonardo Ulloa na Daniel Amartey.

Young Africans Watoa Kauli Kuhusu Mgomo Wa Wachezaji
Kaburi la Faru John ‘Hola..!’