Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka makada wake kuacha tabia ya kulalamika pindi wanapotenguliwa kwenye nafasi zao walizoteuliwa na Rais.
 
Hayo yamesemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu, Ngemela Lubinga alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu vilivypo mjini Iringa.
 
Amesema kuw makada walioteuliwa na Rais na kisha kuondolewa katika nafasi walizopewa waache kupiga kelele au kulalamika, bali wakubali mabadiliko kwa nia ya kuheshimu busara za Ikulu kwa maamuzi yaliyofanywa dhidi yao.
 
“Rais anapoteua viongozi wake kuwapa dhamana anaona kwamba wewe anakuhitaji katika nafasi hiyo na mazingira yaliyopo yanakuhitaji kwa wakati huo lakini inapofika wakati anakuondoa, ujue kwamba mazingira yale huwezi kuyamudu na anakuokoa ili usipate laana,” amesema Lubinga.
 
Hata hivyo, Lubinga amesema kuwa hivi sasa, CCM imejipanga zaidi kimkakati kuhakikisha kuwa inajenga nidhamu na uwajibikaji ndani ya Serikali iliyoingia madarakani kwa tiketi yake kupitia uchaguzi mkuu uliopita.

Magazeti ya Tanzania leo Aprili 18, 2017
Twiga maarufu Duniani azaa