Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema kuwa ujio wa ndege mpya za kisasa utaongeza hali ya amani na usalama katika viwanja vya ndege kwa kuimarisha mifumo mbalimbali ya usalama.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam jana mara baada ya kuwasili kwa ndege mpya, ambapo amesema kuwa ujio wa ndege hizo utaimarisha huduma za usafiri wa anga ndani na nje ya nchi, kitu ambacho kilikosekana kwa muda mrefu.

”Ujio wa ndege hizi kwanza kabisa utakuwa kivutio kwa watalii, ambapo naimani kabisa idadi yao itaongezeka baada ya kuwa na usafiri wenye uhakika, hivyo kulingana na ongezeko hilo, tutaweza kuongeza uimarishaji maradufu wa usalama katika viwanja vya ndege,”amesema Lugola

Hata hivyo, Lugola amewataka wananchi kuwapuuza baadhi ya watu ambao wamekuwa wakibeza jitihada za rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli za kuiletea nchi maendeleo na kusema kuwa waachwe kama walivyo.

Mlipuko wa mafuta waua 12
Kunguni wageuka tishio Kirando

Comments

comments