Mshambuliaji Luis Suarez amekoleza ushawishi kwa viongozi wa FC Barcelona ili wafanikishe usajili wa beki wa pembeni kutoka nchini England na klabu ya Stoke City Glen Johnson.

Gazeti la The Daily Mail limeripoti kuwa, mshambuliaji huyo amekua mstari wa mbele kuushawishi uongozi wake ili ukamilishe mpango huo, kwa kisingizo cha kumfahamu vyema Johnson ambaye alicheza nae katika klabu Liverpool.

Johnson amekua katika orodha ya wachezaji wanaopewa nafasi kubwa kusajiliwa Camp Nou kwa lengo la kuziba pengo lililoachwa wazi na Dani Alves ambaye aliihama FC Barcelona na kutimkia kwa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC.

Tayari meneja wa Barca Luis Enrique, ameonyesha kutoridhishwa na uwezo wa Aleix Vidal ambaye amepewa jukumu la kucheza katika nafasi ya beki wa kulia, jambo ambalo linaendelea kumpa msukumo wa kufanya usajili itakapofika mwezi januari mwaka 2017.

Memphis Depay Kutimka Old Trafford
NATO: Trump sio chaguo la ulaya na Marekani