Msanii wa Bongo Flava, Madee ameweka wazi alipoitoa nguvu kubwa ya kufanikiwa kuishi na rapa toka Ngarenaro, Arusha, Dogo Janja kama mtoto wake.

Madee alifunguka wikendi iliyopita kwenye kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm kuwa mwanamke aliyempenda sana, anayefahamika kwa jina la Pendo ambaye ametangulia mbele ya haki, alikuwa na ndoto ya kuishi naye akiwa na mtoto wa Madee ambaye hakuzaa naye lakini akaahidi angemtunza kwa moyo kama mwana aliyemzaa.

“Ndoto hiyo bahati mbaya hakuitimiza. Lakini mimi ninaiendeleza, kama vile unavyoona sasa hivi naishi na Dogo Janja kama mwanangu,” alisema Madee.

Madee ni baba wa mtoto ambaye alitofautiana na mama yake kwa kipindi kirefu, lakini ameeleza kuwa baada ya kufikia umri unaokubalika, hivi sasa amekabidhiwa mtoto huyo na anampa malezi anayostahili.

Madee akipiga 'selfie' na mtangazaji wa The Playlist, Lil Ommy

Madee akipiga ‘selfie’ na mtangazaji wa The Playlist ya 100.5 Times Fm, Lil Ommy

Msanii huyo pia aliweka historia kwa mara ya kwanza kutambulisha video ya wimbo wake mpya wa ‘Migulu Upande’ kwenye kipindi hicho cha radio badala ya kutumia runinga kama ambavyo ilitengemewa na wengi.

“Nimeamua kuitambulisha video yangu kwenye The Playlist ya 100.5 Times fm kwa sababu najua ni show kali inayoheshimika sana na ya kibabe. Baada ya dakika 15 itapanda YouTube na TV” alisema Madee, baada ya kuichambua nje ndani video yake kwa lugha ya picha kwenye kipindi hicho cha radio.

Leicester City Kutembeza Kombe La Ubingwa Wa EPL Barabarani
Waziri Mkuu aweka sawa ‘Bunge kurushwa Live’

Comments

comments