Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, imetoa amri kuwa wabunge wanne wa chama cha upinzani Chadema wakamatwe kwa kosa la kukiuka masharti ya Mahakama.

Wabunge hao ambao wamekiuka masharti ya dhamana ni Ester Bulaya (mbunge wa Bunda mjini), Halima Mdee (Mbunge wa Kawe),  Peter Msigwa (Mbunge wa Iringa Mjini), na John Heche (Mbunge wa Tarime Vijijini).

Amri hiyo imetolewa leo kufuatia washtakiwa hao kutofika Mahakamani hapo bila kuwepo kwa taarifa zozote kutoka kwao wala wadhamini wao wakati kesi yao ilipofika  kwaajili ya kusikilizwa.

Wabunge hao wanne walikamatwa na kushtakiwa katika kesi ya uchochezi namba 112 ya mwaka 2018.

Ikumbukwe kuwa Novemba 13, 2018 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe pamoja na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko walifutiwa dhama katika kesi yao ya uchochezi baada ya kusafiri nje ya nchi bila kibali cha Mahakama.

Mtoto wa miezi mitano atelekezwa 'guest' na ujumbe
MOI yafanikisha upasuaji mtoto mwenye kifafa