Taarifa ya bodi ya madaktari wa timu ya Taifa ya Misri imethibitisha kuwa mchezaji wa Liverpool, Mohamed Salah mwenye  miaka 27 hali yake haipo sawa.

Salah ana maumivu ya ‘enka’ ambayo aliyapata kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Crystal Palace hali iliyomlazimu aukose mchezo dhidi ya Manchester United.

Kiongozi wao Dr.Mohamed Abul-Ela amethibitisha kwamba bado Salah hajawa tayari kucheza mechi za ushindani kwa sasa.

“Mchezaji alikuja kambini Jumanne jioni akawa chini ya uangalizi hata alipokuwa akifanya mazoezi uwanja  wa Burj Al Arab alikuwa kwenye uangalizi,” ilieleza taarifa hiyo.

Salah atakosa mchezo dhidi ya Kenya na Comoro ambayo ni maalumu kwa ajili ya michuano ya Afcon kwa kuwa anahitaji muda mrefu kurejea kwenye ubora.

Wakulima Mtwara wauawa na watu wasiojulikana
Bunge lapitisha wanaoambukizwa Ukimwi kulipwa fidia