Mjumbe wa Kamati Kuu ya  Taifa (NEC)  ya CCM, Januari Makamba, anatarajiwa kuunguruma katika mkutano wa hadhara utakaofanyika katika Misufini,Jimbo la Dimani,Mjini Unguja.

Aidha, huo ni muendelezo wa kampeni za uchaguzi mdogo wa marudio ya ubunge katika Jimbo laDimani, unaotarajiwa kufanyika januari 22, mwaka huu.

Hata hivyo, katika mkutano huo Makamba anatarajiwa kumnadi mgombea ubunge jimbo la dimani kwa tiketi ya CCM, Juma Ali Juma ambaye anaonekana kukubalika zaidi na wananchi wengi jimboni humo.

“Natoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika mktano huu mhimu kwani  utafanyika nyumba kwa mgombea wa CUF, hivyo tunaenda kusambaratisha ngome yake,”amesema Mgeni.

Kwa upande wake Naibu Katibu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai amewataka wana CCM kujiepusha na watu wenye hila ovu ya kuleta mchafuko .

 

Lembeli aiponda tume ya kuchunguza faru John
Masele: kwa heri ukapera