Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amezuia utekelezaji wa agizo lililotolewa hivi karibuni na Jeshi la Polisi mkoani humo kuwa magari yote yenye vioo vyeusi visivyoonesha ndani (tinted) wanapaswa kuziondoa.

Makonda amesema kuwa amelazimika kusitisha agizo hilo lililotolewa awali na jeshi la polisi kwani litaleta usumbufu mkubwa kwa waakaazi wa jiji hilo na wageni wanaotoka mikoani ambako zuio hilo halikuwaathiri.

“Tunafahamu kuwa wapo akina mama ambao wanaweka tinted kama sehemu ya kujilinda ili wale wezi wa magari wasije wakawaona kuwa ni akina mama tu wakawakimbiza na kuwanyang’anya magari yao,” alisema Makonda.

“Nasitisha zoezi la ukamataji wa magari yenye tinted lililokuwa linatakiwa kufanyika kesho na jeshi langu la Polisi mkoa wa Dar es Salaam mpaka nitakapopata hoja za msingi za kujiridhisha dhidi ya zoezi hili,” aliongeza.

Alisisitiza kuwa ana imani kubwa na jeshi la polisi hivyo halitashindwa kuwadhibiti watu wachache ambao wanaweza kutumia tinted kama kichaka cha kuharibu matumizi ya vioo vya aina hiyo kwa watu wema.

Agizo la kuondoa tinted lilipaswa kuanza kutekelezwa leo, Agosti 7.

Lulu ataja kinachozimaliza filamu za kitanzania
LIVE: Rais Magufuli akizindua stendi ya mabasi Korongwe, Tanga