Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewapa miezi tisa wafanyabiashara wa magari kuhamia Kigamboni kwenye eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya biashara hiyo.

Ameyasema hayo hii leo jijini humo ambapo amesema kuwa ifikapo Oktoba mwaka huu hataki kuona mfanyabishara yeyote wa magari katika maeneo ya jiji hilo na kutaka ifikapo mwezi huo wote wawe wameshahamia Kigamboni.

“Ikifika mwezi huo wa tisa ambao ni mbali kweli lakini ni karibu sana, mimi akili yangu nilikuwa nafikiri niwape mpaka mwezi wa sita maana yake una muda wa kujipanga saizi ila mwezi wa tisa nisikute mtu katika maeneo haya ya Jiji,”amesema Makonda.

Aidha, Makonda amemuagiza Afisa Biashara kuhakikisha kuwa hakuna mfanyabiashara ambaye ataweza ku ‘renew’ leseni yake akiwa mjini bali anatakiwa aweze kufanya zoezi hilo na kuhesabika akiwa Kigamboni.

Azam, Yanga kupigwa saa 10 Chamazi
Msigwa na wenzake 12 wafikishwa mahakamani