Wajasiliamali Jijini Dar es salaam wametakiwa kuhakikisha wanatumia vyema mafunszo waliyopatiwa kutoka Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo Nchini (SIDO).
 
Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Jiji, alipokuwa akifunga mafunzo ya siku tano kwa wajasiliamali yanayoendeshwa na Sido kwa ajili ya kuwawezesha wajasiliamali wadogo wadogo kuweza kusindika na kuongeza thamani bidhaa mbalimbali.
 
“Sisi kama Jiji tumeandaa mpango kabambe wa utalii wa mkoa wa Dar es Salaam ambao utaweza kuwasaidia wajasiliamali wa ndani kuuza bidhaa zao, hivyo kila mjasiliamali ahakikishe anajiandaa kwa kuandaa vitu vyake katika ubora unaohitajika” amesema Lyana.
 
Aidha, ameweka wazi kuwa kama wajasiliamali wote hao wataweza kufanya kama walivyofundishwa wataweza kumsaidia Rais juu ya kuipelekea nchi katika uchumi wa kati ambao unategemea sana Viwanda.
 
  • Ubadhirifu mkubwa wabainika Shirika la Posta
  • Chupi anasa mkoani Lindi
  • Majaliwa aagiza Wakurugenzi wachunguzwe
 
Hata hivyo, ametoa wito kwa wadau na watu wengine kwenda kujifunza Sido ili iwe rahisi kurasimisha biashara zao ambazo walikuwa wanafanya kienyeji

UVCCM: Wametuletea mtu mwenye historia ya kushindwa
Majaliwa: Hakikisheni mnatokomeza uvuvi haramu