Klabu ya Manchester United imepanga kutumia Pauni 50 milioni tu kwenye usajili wa kiungo mshambuliaji wa England na Chelsea, Mason Mount kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya.

Staa huyo wa Stamford Bridge amebakiza mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake huko Chelsea.

The Blues wanataka mchezaji wao abaki, lakini dili jipya halionekani kufikiwa kabisa na Man United imeonyesha dhamira ya dhati ya kumsajili, lakini ofa yao ni Pauni 50 milioni tu.

Chelsea inahitaji ilipwe Pauni 70 milioni kwenye mauzo ya kiungo huyo, lakini Man United wao kiwango cha pesa walichopanga kutumia kwenye kunasa saini ya mchezaji huyo ni Pauni 50 milioni.

Man United imekuwa ikihusishwa na nyota huyo kwa muda mrefu na sasa wanataka kulitumia dirisha hili kumnasa ili kuimarisha kikosi chao na kwa Kocha Erik Ten Hag anataka kufanya panga pangua ili kutengeneza kikosi cha ubingwa msimu ujao.

Tayari Man United imeshaweka mezani baadhi ya majina ya nyota itakaowaacha na inahusioshwa na majina mengine makubwa ikiwamo Neymar na Harry Kane.

Ten Hag anaamini mabosi wa timu hiyo watamwaga pesa ya kutosha kwa ajili ya usajili na hilo likitimia na kunasa mastaa hao, msimu ujao miamba hiyo ya Manchester itakuwa moto ikiwania ubingwa.

Chelsea yaingilia dili la Moses Caicedo
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 7, 2023