Afisa habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara amewaonya mashabiki wa Simba kuacha mara moja kuwazomea mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga katika mchezo wa kimataifa dhidi ya St. Louis siku ya Jumamosi.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema anawaomba mashabiki soka nchini kuziunga mkono timu zao za nyumbani Simba na Yanga kama timu zinazo wakilisha nchi na kuacha tamaduni za kuzomeana na kuvunjana moyo.

“Natoa wito kwa washabiki wa Simba watakaoenda uwanjani kwenye mechi ya Yanga Jumamosi wasiizomee,tuzomeane kwenye ligi ya nyumbani. Sisi sote ni watanzania na tunawakilisha nchi,”amesema Manara

Hata hivyo, timu ya Simba inatarajiwa kushuka dimbani siku ya Jumapili (Februari 11, 2018) kuvaana na Gendemerie Nationale katika mchezo wao wa kimataifa huku  Rais wa awamu ya pili Al Haji Hassan Mwinyi kuwa mgeni rasmi wa mechi hiyo.

Evra mambo safi West Ham Utd
Video: Mgombea Ubunge wa CUF Kinondoni adai kumuunga mkono JPM