Hatimaye Uongozi wa Klabu ya Young Africans umemtambulisha rasmi Mshambuliaji kutoka DR Congo Fiston Mayele.

Mayele ametambulishwa kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za klabu hiyo kwa kuweka Video maalum ya utambulisho.

Katika Video hiyo Mayele anaonekana akiwa amevaa Jezi namba 9, ambayo ataitumia ndani ya kikosi cha Young Africans kuanzia msimu ujao wa 2021/22.

Kichwa cha taarifa iliyowekwa kwenye kurasa za klabu ya Young Africans kinasomeka ‘Fiston Mayele is now 𝗚𝗥𝗘𝗘𝗡 AND 𝗬𝗘𝗟𝗟𝗢𝗪’.

Mayele aliwasili nchini jana Jumamosi (Julai 31) akitokea nchini kwao DR Congo alipokua akiitumikia AS Vita Club.

Young Africans yaanza kwa sare Kagame Cup
Tanzania kupata chanjo milioni 11 - Msigwa