Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, James Mbatia amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kudhibiti vitendo vya rushwa, uhalifu, utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya reli ya kisasa, upatikanaji wa elimu bure.

Mbatia ambaye pia ni mbunge wa Vunjo amesema hayo leo Julai 27, 2019 jijini Dar es Salaam katika mkutano mkuu wa chama hicho kwa ajili ya kuchagua viongozi wapya wa chama hicho.

Amepongeza Serikali na hatua nyingine kadhaa ikiwemo uthubutu wa kutekeleza mambo mbalimbali katika kipindi cha miaka minne tangu Rais Magufuli alipoapishwa Novemba 5, 2015.

“Rais Magufuli ni mwenye uthubutu na amefanya makubwa yenye uthubutu hata wengine hawawezi kufanya.”

Aidha, Mbatia amemuomba Rais Magufuli aridhie uwepo wa meza ya maridhiano ya vyama vya siasa ili kujenga nyumba moja.

“Basi athubutu kutukalisha tuzungumze ili tuwe na mifumo imara na taasisi imara na endelevu kwa maslahi mapana ya mama Tanzania, mimi niko tayari tuyazungumze,” amesema Mbatia.

Sakata la rushwa la DC Sabaya latua kwa RC Mghwira
LIVE JIJINI DAR ES SALAAM; Mkutano Mkuu wa NCCR MAGEUZI wakichagua viongozi wapya

Comments

comments