Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara amejikuta akimwaga machozi mbele ya Waandishi wa Habari bada ya kutoa maelezo ya kuilalamikia Serikali ya Mkoa wa Mara kushindwa kumshirikisha katika zoezi la uwekaji wa alama za mawe ya mipaka kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Waitara, amejikuta katika hali hiyo alipokuwa akitoa malalamikio hayo wakati akizungumza na vyombo vya Habari hii leo Machi 28, 2023 jijini Dodoma na kusema hatua hiyo inatokana na malalamiko ya watu waliokuwa wakiishi katika eneo hilo ambao wametendea mambo yasiyofaa.

Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara.

Waitara ameongeza kuwa, awali walikubaliana na Serikali ya mkoa wa mara juu ya zoezi hilo la uwekekaji wa vigingi lakini cha kushangaza zoezi hilo linaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Seleman Mzee, limeanza bila kumshirikisha Mbunge wa jimbo na kusema hawezi kuliunga mkono.

Hata hivyo, Mkuu wa mkoa wa Mara, Meja Jenerali Seleman Mzee amesema utekelezaji uwekaji wa vigingi hivyo linaenda kwa kufuata maelekezo ya Kamati ya Mawaziri wanane, ambao walizunguka maeneo zaidi ya 97 yenye migogoro.

Fursa ujio Makamu wa Rais wa Marekani nchini
TANAPA kujiuliza matumizi fedha za UVIKO-19