Kansela wa Ujerumani, Angel Merkel  amesema kuwa anaunga mkono mashambulizi ya kijeshi yaliyofanywa na Marekani, Ufaransa na Uingereza nchini Syria akiyataja kuwa ni muhimu na yanayostahili.

Wiki hii Kansela Merkel alitoa tamko kuwa Ujerumani haitashiriki katika hatua za kijeshi dhidi ya Syria lakini anaunga mkono hatua za kijeshi zinazochukuliwa na nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Kwa upande wake, Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May amesema kuwa mashambulizi hayo ya Syria ni halali kwa sababu wanaushahidi kuhusu silaha za kemikali zilizotumiwa na Syria.

Aidha, Ufaransa imesema kuwa ilifyatua makombora 12 yaliyolenga maeneo kadhaa ya jeshi la Syria na kuongeza kuwa watafanya mashambulizi zaidi iwapo silaha za sumu zitatumika tena Syria.

Hata hivyo, Waasi wa Syria wamesema kuwa mashambulizi hayo ya kijeshi yatakuwa hayana maana kama hayatalenga kumuondoa madarakani Rais Bashar al Assad.

Urusi, Syria zaitaka Marekani isubiri matokeo ya mashambulizi
Uamuzi wa Basata dhidi ya Bill Nas na Nandy