Mshambuliaji kutoka nchini Zimbabwe na klabu ya Azam FC Prince Mpumelelo Dube, amerejea kwenye mbio za kusaka tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21, baada ya kimya cha muda mrefu.

Dube alifunga bao lake saba msimu huu, ikiwa ni bao lake la kwanza tangu mwaka huu 2021 ulipoanza, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City uliochezwa jana usiku Uwanja wa Azam Complex Chamazi, jijini Dar es salaam.

Mshambuliaji huyo ambaye alianza kwa kasi kubwa ya kuzifumania nyavu mwanzoni mwa msimu huu, alifunga bao la pili na la ushindi kwa Azam FC katika mchezo huo dhidi ya Mbeya City, huku bao la kwanza la wanalambalamba hao wa Dar es salaam likifungwa na Iddy Suleyman ‘NADO’ na bao la kufutia machozi la Mbeya City likapachikwa wavunji na David Mwasa.

Kwa juhudi za kufunga bao lake la sita msimu huu, kunamfanya Dube kuwa nyuma kwa mabo matatu dhidi ya kinara wa ufungaji wa mabao msimu huu Meddie Kagere ambaye tayari ameshaingia nyavuni mara tisa.

Wengine walio kwenye orodha hiyo ni John Bocco – Simba ana mabao manane, Adam Adam (JKT Tanzania), Meshack Abraham (Gwambina FC) wana mabao saba kila mmoja.

👉Clatous Chama Magoli 6️⃣🦁
👉Deus Kaseke Magoli 6️⃣
👉Yusuph Mhilu Magoli 6️⃣
👉Raidhin Hafidhi 5️⃣
👉Seif Abdallah Magoli 5️⃣
👉Fully Maganga Magoli 5️⃣
👉Ayoub Lyanga Magoli 5️⃣
👉Chris Mugalu Magoli 4️⃣🦁
👉Reliantis Lusajo Magoli 4️⃣
👉Yacouba Sogne Magoli 4️⃣
👉Obrey Chirwa Magoli 4️⃣
👉Bigirimana Blaise Magoli 4️⃣
👉Michael Sarpong Magoli 4️⃣
👉Lamine Moro Magoli 4️⃣
👉Deogratius Mafie Magoli 4️⃣
👉Daniel Lyanga Magoli 4️⃣
👉Kibu Denis Magoli 4️⃣
👉Iddy Nado Magoli 4️⃣

Ihefu FC yazika hofu ya kushuka daraja
Baraza: Sijali kufungwa, nimependa tulivyocheza