Beki Tyrone Mings amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitimikia AFC Bournemouth inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini England kwa msimu wa pili mfululizo, tangu ilipopanda daraja ikitokea ligi daraja la kwanza mwaka 2016.

Mings amesaini mkataba wa miaka miwiwli ambao utamuweka klabuni hapo hadi mwaka 2019. Mings alijiunga na AFC Bournemouth akitokea katika klabu ya Ipswich Town inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England mwaka 2015, lakini hakubahatika kucheza michezo kadhaa ya ligi msimu uliopita kutokana na majeraha ya goti yaliyomkabili kwa muda mrefu. Beki huyo mwenye umri wa miaka 24, alicheza michezo 7 pekee msimu uliopita.

“Yalikua maamuzi sahihi kwetu na kwa mchezaji kwa ujumla, tunaamini kukamilika kwa dili hili la kusaini mkataba mpya kutafungua ukurasa mpya kwa Mings na kwetu pia,” imeeleleza taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya AFC Bournemouth. (www.afcb.co.uk)

Ming naye akahojiwa na tovuti hiyo na kueleza kuwa “Miaka yangu miwili tangu niliposajiliwa klabuni hapa, haikuwa rahisi kufikia malengo ya kucheza soka kama nilivyotarajia kutokana na changamoto za majeraha, lakini sasa naamini muda wa miaka mingine miwili nilionao, nitafanya jitihada kwa kushirikiana na wenzangu kufikia malengo ya klabu hii.”

Mings anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha AFC Bournemouth kitakachopambana na Arsenal siku ya jumamosi, katika mchezo wa mzunguuko watatu wa ligi kuu ya soka nchini Engalnd.

Dirisha la usajili Uturuki kumuokoa Jack Wilshere
Majareha yamuweka shakani David Alaba