Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amesema kuwa ili kudhibiti ukataji miti ovyo, Serikali  imekusudia kupandisha kodi ya Nishati ya mkaa.

Maghembe amesema hayo huku akieleza kwamba asilimia 93 ya Watanzania wanatumia nishati ya mkaa na kuni, hivyo wanahitaji mvua na hewa safi ili kuishi, hivyo kuwa na kila sababu ya kutafuta njia ya kupunguza ukataji miti.

Aidha, Maghembe alisema kuwa hatua hiyo ya kupandisha bei ya mkaa  itasaidia watu kupunguza matumizi ya nishati hiyo na kupunguza ukataji miti hovyo.

“Nafikiri tukipandisha kodi ya mkaa,lazima utapanda bei maradufu, hivyo idadi ya watu wanaokata miti kwaajili ya uuzaji wa mkaa,hapo tutakuwa tumeokoa misitu yetu”alisema Maghembe.

Hata hivyo Maghembe amesema Serikali inatafuta njia ya kupunguza matumizi ya mkaa kwa sababu ukataji miti unatishia uhai wa watanzania kutokana na ukweli kwamba ukataji miti unasababisha ukame na joto, hivyo si jambo jema.

Rais Magufuli: Sitaki Majeshi yaingie ubia na watu binafsi
Sirro atangaza kiama kwa vibaka na wahalifu Dar