Kiasi cha Shilingi Bilioni 2, kilichotengwa na Serikali kwa ajili ya mikopo kimeanza kufanya kazi baada ya Mfanyabiashara Shaban Ally kupatiwa mkopo wa Shiling Milioni 50 na Waziri wa Nishati, January Makamba zitakazomsaidia kukuza biashara yake ya Mafuta.

Waziri Makamba, ambaye bado yuko kwenye ziara ya Kijiji kwa Kijiji ametoa kiasi hicho cha pesa mara baada ya kuzungumza na Wananchi, wakati akiwa katika Kijiji cha Ugaka kilichopo Wilayani Igunga Mkoani Tabora.

Waziri wa Nishati, January Makamba akishuhudia namna ambavyo mfanyabiashara Shaban Ally akitekeleza majukumu yake.

Shaban Ally, ni Kijana ambaye anafanya biashara ya mafuta ya kupima kwenye chupa na madumu kwenye Kijiji hicho na kabla ya kupatuwa mkopo huo pia alipata wasaa wa kuzungumza na Waziri huyo wa Nishati.

Waziri Makamba amesema, “Basi sisi tutakukopesha Milioni 50, maana tumetenga Bilion 2 kama sehemu ya majaribio kwa mwaka huu wa fedha sababu ni kwamba Wananchi Vijijini wanateseka kupata mafuta ambayo si salama na kwa bei ya juu.”

Zoran Maki afichua uwezo wa Mohamed Ouattara
Mugalu atoa ya moyoni Simba SC